Back to top

Meli ya mizigo ya Urusi yashindwa kuendelea na safari sababu ya upepo.

18 December 2018
Share

Upepo mkali uliokuwa unavuma eneo la kusini magharibi mwa fukwe ya Cornwall nchini Uingereza umeikokota meli ya mizigo ya Urusi ya Kuzma Minin  na kuipeleka ufukweni na hivyo kushindwa kuendelea na safari mapema alfajiri hii leo.

Kitengo cha huduma za dharura za uokozi nchini Uingereza kimeanza jitihada za kuinasua meli hiyo iweze kuendelea na safari yake.

Taarifa zinasema kuwa ndani ya meli hiyo ya mizigo  kuna wafanyakazi wasiopungua 18 na kwamba haikuwa imebeba mzigo ndani yake.