Back to top

Chanzo kipya cha maji kumaliza changamoto ya majisafi na salama Mwanza

03 January 2019
Share

Ujenzi wa chanzo kipya cha maji safi eneo la Butimba wilayani Nyamagana jijini Mwanza ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za ujazo 40,000 kwa siku, ambao ni miongoni mwa sehemu tano za mradi wa kuboresha majisafi na mazingira katika ziwa Victoria, unatarajia kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo ya jiji la Mwanza, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayapati huduma ya uhakika ya maji.


Maeneo yatakayohudumiwa na chanzo hicho cha maji ni pamoja na Nyegezi, Buhongwa, Iwanima, Sahwa, Kishiri, Isangijo , Kisesa na Usagara. 


Kukamilika kwa ujenzi wa chanzo hicho kutasaidia kutatua changamoto ya wakazi wa maeneo hayo kupata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia zaidi ya 90. 


Mbunge wa jimbo la Nyamagana  Mhe.Stanslaus Mabula amewahimiza wakazi wa maeneo yote ambayo miradi hiyo itapitia  kuhakikisha wanatoa fursa ya kuachia maeneo yao kwa ajili ya kupitisha mabomba ili miradi hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi.