Baadhi ya wananchi kutoka kata ya Mjimwema wilayani Njombe mkoani Njombe ,wameelezea kuridhishwa na ukamatajwa wa watuhumiwa 28 wa mauaji ya watoto wilayani humo katika oparesheni inayoondeshwa na kikosi utendaji cha operasheni na mafunzo cha Jeshi la polisi huku wakiwaomba wenzio wasijichukulie sheria mkononi kukabiliana na tatizo hilo.
Siku za hivi karibuni kumejitokeza aina nyingine ya mauaji ya watu watatu yanayodaiwa kutekelezwa na wananchi kwa kujichukulia sheria mkononi na kuwaua watu wanaohisiwa au kutuhumu kuwa huenda ndio vinara wanaotekeleza matukio ya utekeji na kuwaua watoto.