Back to top

Kampeni ya nyumba kwa nyumba kufanyika kutokomeza ugonjwa wa ukoma.

25 November 2019
Share

Wizara ya afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma inakusudia kuendesha kampeni ya nyumba kwa nyumba  kwa ajili ya kutokomeza  ugonjwa wa ukoma katika maeneo  ya wilaya zilizobainika bado kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ugonjwa huo.

Akizungumza jijini Arusha wanapokutana wadau wa afya wanaoshiriki kwenye mpango wa taifa wa  kutokomeza kifua kikuu na ukoma nchini Meneja wa mpango huo dakta Beatrice Mutayoba anasema kampeni hiyo itaelekeza nguvu kwenye halmashahuri kumi na sita zilizobainika kuwa bado na  wagonjwa.

Dakta Leonard Subi ni Mkurugenzi wa kinga Wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,wazee jinsia na watoto amesema mpaka sasa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu nchini imefikia asilima hamsini na tatu pekee.