Katika harakati za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeridhia kwa baadhi ya taasisi zake kutoa likizo za lazima ili kupunguza msongamano na mikusanyiko maofisini.
Habari ambazo ITV imezipata tayari baadhi ya wizara za serikali zimeanza utaratibu wa kuwapa likizo za lazima wafanyakazi huku baadhi ya mashirika wafanyakazi wakibadilishana na wenzao baada ya siku kumi huku Mfanyakazi wa ZSTC Ali Meraji amekiri kupewa agizo la kubaki nyumbani.