![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/fisi.jpg?itok=_FCZ9Xxj)
Wananchi wa kata ya Ngongwa Msalala wilayani Kahama wamelalamikia kusumbuliwa na fisi wakati wakienda kutafuta maji katika visima vilivyoko mbali na makazi yao kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya majisafi na salama katika eneo lao.
Malalamiko hayo yametolewa na wananchi wa Kata ya Ngongwa katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama wakati kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikitembelea na kukagua miradi ya maji inayojengwa kwa ubia wa nguvu za wananchi na serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wamazingira Shinyanga (SHUWASA) Bi. Flaviana Kifizi ameainisha kuwa changamoto ya uhaba wa maji unaolalamikiwa na wakazi wa eneo hilo itamalizika mwezi Agosti mwaka huu baada ya mradi mkubwa wa maji wa shikingi bilioni 2.4 kukamilika.