Back to top

Serikali kupambana na unyanyasaji na mauaji ya wazee nchini.

01 October 2020
Share

Serikali imesema itaendelea kupambana na unyanyasaji wa wazee nchini ikiwemo kudhibiti vitendo vya mauaji ya wazee.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.JOHN Jingu alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.

Dkt.Jingu amesema serikali inafanya jitihada za kuwatunza wazee hasa wasiojiweza kwa kuboresha makazi ya wazee yanayosimamiwa na serikali.

Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dodoma wakizungumza katika nyakati tofauti wamesisitiza kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 28 mwezi huu.