Back to top

Mwinyi ala kiapo kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Tanzania.

16 December 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Husein Mwinyi leo amekula kiapo cha kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dr.Mwinyi amekula kiapo hicho mbele ya jaji mkuu profesa Ibrahimu Juma na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli na kisha kuhudhuria kikao cha kwanza cha baraza hilo.

Akifungua kikao hicho Rais Dr. Magufuli amempongeza Dr. Mwinyi kwa kuwa mjumbe wa baraza hilo na kuwapongeza mawaziri wote kwa kuanza vyema kutimiza wajibu wao wa kuzisimamia wizara walizopewa kuziongoza.

Kikao hicho kinaendelea kufanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma chini ya uenyekiti wa Rais Dr. Magufuli.