Back to top

Bei ya mafuta ya kupikia mwiba kwa mama ntilie Mtwara.

24 January 2021
Share

watumiaji wa mafuta ya kula wakiwemo mama nitilie katika manispaa ya mtwara mikindani wameiomba serikali kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula katika viwanda vya ndani,  ili kuondokana na upungufu wa bidhaa hiyo inayopelekea kupanda na hivyo kuyumbisha biashara za wajasiria mali wadogo.
.
wamesema kwa sasa ndoo ndogo ya mafuta ya kula iliyokuwa ikiuzwa kwa bei ya shilingi elfu thelathini na mbili imepanda na kufikia shilingi elfu arobaini na tano kiwango ambacho ni kikubwa.
.
hivyo wameiomba serikali kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula kipindi hiki ili kuondokan a na bei hizo ambazo ni kubwa na zinatishia ustawi wa biashara zao kwa sasa.
.
kwa upande wao baadhi ya wauza maduka ya mafuta hayo wamesema wanalazimika kupandisha bei kutokana na mafuta hayo kupanda licha ya wateja kulalamikia bei hiyo.