Back to top

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ateta na Waziri wa Sweden.

28 May 2021
Share

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Ndugu Janine Alm Ericson.

Mazungumzo hayo ya Waziri huyo na Vyama Vikuu vya Upinzani Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es salaam yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA Ndugu Ndugu Rodrick Lutembeka na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Ndugu Anders Sjoberg.

Mazungumzo yaliangazia hali ya kisiasa nchini Tanzania na hatua zinazochukuliwa/zinazopaswa kuchukuliwa kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini Tanzania.