Back to top

Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Morogoro.

06 July 2021
Share


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro Jumatano, Julai 7 mwaka huu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili katika maeneo ya Msamvu manispaa ya Morogoro, Dumila wilayani Kilosa na wilaya ya Gairo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Martin Shighela amesema ziara hiyo ya kwanza ya Mhe.Samia Suluhu Hassan tangu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itahusisha mikutano na wananchi hivyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wao.

Katika ziara yake, Mhe.Rais Samia pia atashiriki mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania utakao fanyika Julai 8 katika manispaa ya Morogoro.