![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/photo_2021-11-10_13-57-10.jpg?itok=HSC04J2x)
Mahakama kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi kupinga maelezo yaliyotolewa na shahidi namba nane kuwa mshitakiwa wa tatu Mohamedi Lingwenya alihojiwa katika Kituo Kikuu Cha Polisi Dar es Salaam na kuandika maelezo ambapo upande wa waweka pingamizi wanasema hakuwahi kuandika maelezo, bali yaliandikwa na yeye akatakiwa kusaini na kwamba hakupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyosema shahidi.