Back to top

Chebukati alifanya kazi kwa kuzingatia katiba

01 September 2022
Share

Wakili wa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya Wafula Chebukati, Prof.Githu Muigai ameiambia Mahakama kuu kwamba, Chebukati alifanya kazi kwa kuzingatia sheria na Katiba ya Kenya, alipomtangaza William Ruto kuwa Rais mteule.
.
Hata hivyo, Katika kujibu rufaa ya Kiongozi wa Chama cha Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga anayetaka mahakama hiyo kufutilia mbali matokeo ya kura za Urais,  Muigai alieleza kuwa, kufanya hivyo kutaashiria kwamba Uchaguzi mzima ufutiliwe mbali.