
Raia 52 kutoka nchi za Rwanda, Congo- DR, India, Uturuki, Somalia, Ethiopia, Uganda, Burundi na Kenya ,wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja mkoani Morogoro, kwa kuingia nchini bila kibali.
.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhamiajimkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Joseph Kasike, ambapo amebainisha kuwa, raia hao wamekamatwa baada ya kuanza kwa kampeni ya mjue jirani yako, na tayari wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria.