Meli ya Kitalii ya Zaandam kutoka Florida nchini Marekani ikiwa katika ziara ya siku 71 ya kutembelea nchi mbalimbali Barani Afrika na vivutio vya utalii Katika nchi hizo, imetia nanga Katika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea nchini Misri ikiwa na watalii 1060 kutoka Mataifa ya Marekani na Ulaya pamoja na Wafanyakazi 520 kutoka Mataifa 35 Duniani.
Watalii hao watakuwa nchini kwa siku Nne ambapo tarehe 10 na 11 Novemba, 2022 watafanya Utalii katika Jiji la Dar es Salaam, Mji wa kale wa Bagamoyo na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na tarehe 12 na 13 Novemba, 2022 watatembelea Visiwa vya Zanzibar.
Ujio wa meli hiyo ambayo ni moja kati ya Meli kubwa za watalii ni matokeo ya Filamu ya "The Royal Tour".