Back to top

IGP WAMBURA ZIARANI BANGKOK, THAILAND

25 November 2022
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, ameendelea na ziara yake ya kikazi nchini Thailand ambapo ametembelea kituo cha simu za dharula kilichopo jijini Bangkok, kinachohusika na kupokea, kuchakata na kusambaza taarifa za Uhalifu na Majanga mbalimbali.


Lengo la ziara hiyo ni kujionea teknolojia inayotumika, utendaji kazi na utatuaji wa changamoto zinapojitokeza ikiwa na nia ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kati ya Jeshi la Polisi Tanzania, Jeshi la Polisi Thailand na Polisi Bavaria ya Ujerumani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye programu ya Miji Salama.