Back to top

RUWASA na DDCA kuwezesha upatikanaji wa maji - Manyara.

01 February 2023
Share

Wakala wa Usambazaji Maji, Usafi na Mazingira (RUWASA) wakishirikiana na Wakala wa uchimbaji visima na mabwawa [DDCA] wameanza kutekeleza zoezi la uchimbaji wa visima 10 kati ya visima 36 vilivyopo katika mpango wa mwaka 2022\2023

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Afisa Masoko na Mahusiano Kutoka [DDCA] Bi. Ashura Katuga amesema lengo la miradi hiyo ni kumtua Mama ndoo kichwani ambapo visima hivyo vitachimbwa katika Mkoa wa Manyara.

Aidha katika Hatua nyingine Bi. Katuga ameishukuru serikali pamoja na Wizara ya Maji kwa kuiwezesha DDCA ili kuanza zoezi la uchimbaji wa visima kwa kutumia mitambo mipya iliyozinduliwa Novemba 11.2022. ambapo Mikoa yote ya Tanzania itafikiwa na huduma ya mitambo hiyo.

Bi. Katuga ameongeza kuwa toka kuzinduliwa kwa mitambo hiyo mpaka sasa tayari mikoa 11 imefikiwa na zoezi la uchimbaji wa visima na katika mkoa wa Manyara tayari visima 10 kati ya 36 vimeanza kutekelezwa katika wilaya ya Babati, Hanang, Mbulu na Kiteto.

Sambamba na utekelezaji wa miradi hiyo pia Bi. Katuga ametoa wito kwa Taasisi za Umma, binafsi na mtu mmoja moja ambao wanauhitaji wa kuchimbiwa visima vitakavyo kidhi mahitaji yao kufika katika ofisi za RUWASA katika mkoa husika.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara Eng. Wolta Kitita amesema wapo tayari kushirikiana kwa pamoja ili kutekeleza miradi ya uchimbaji wa visima kwa kuzingatia ufanisi wa DDCA katika matokeo ya miradi hiyo  ili Kutatuwa changamoto ya upatikanaji wa maji.