Back to top

WALIOFUTIWA MITIHANI KIDATO CHA 4 KURUDIA

12 April 2023
Share

Wizara ya Elimu imetoa maelekezo kwa wanafunzi 337 wa kidato cha nne mwaka 2022 ambao matokeo yao yalifutwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu na kuandika matusi, kuomba kurudia tena mitihani hiyo.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Wizara hiyo, Prof.Adolf Mkenda, na kubainisha kuwa utaratibu wa kurudia mitihani hiyo kwa wanafunzi hao utakwenda sambamba na mitihani ya kidato cha sita ambayo inatarajiwa kuanza Mei 02,2023, ambapo wanafunzi hao watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia mitihani hiyo.