
Mtu mmoja amefariki huku wengine wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari 5, yakiwemo malori 3 na basi la abiria, mali ya kampuni ya Johanvia, lenye namba za usajili T 728 EBT lililokuwa likitokea Musoma kwenda mkoani Dar es Salaam, katika eneo la Kingoliwira nje kidogo ya mji wa Morogoro.
.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mororogoro, ACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori la mafuta kuhama njia na kulifata basi.