![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/NNGUVU%20KIUME.jpg?itok=Ih4In9aV)
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya BLK iliyopo nchini India, imesema imeanzisha huduma mpya ya kuzibua mishipa ya damu iliyoziba na kusababisha YA KUTIBU matatizo ya kupungua kwa nguvu za kiume, ili kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo hayo.
.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Peter Kisenge, wakati akizungumza na waandishi wa habari, juu ya kambi maalumu ya matibabu ya siku tano inayofanywa na madaktari Bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na mwenzao wa Hospitali ya BLK.