
Kutokana na Mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hamas kupamba moto, Serikali ya Tanzania imesema imeandaa mpango wa kuwarejesha Watanzania waliopo nchini Israel na maeneo mengine ya karibu.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyotumwa kwa vyombo vya habari, imeelekeza kwa Watanzania walio tayari kurejea nyumbani kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe [email protected] au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa 6 usiku.