Back to top

ACHENI KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI - RAIS SAMIA

13 July 2024
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi kuacha kuvunja sheria kwa kuvamia maeneo ya hifadhi na badala yake kutunza mazingira hayo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mlele, Kata ya Inyonga Mkoani Katavi.

Amesema "Tunajua kuna uhaba wa Ardhi na kuna maeneo ya hifadhi mnayatamani lakini hayaendani na kuvunja sheria tukae tuzungumze tuangalie namna ya kuyamega na si kuvamia" amesisitiza Mhe. Rais Samia.

Kauli hiyo imekuja kutokana na maombi ya Mbunge wa Mlele, Mhe.Isack Kamwelwe aliyeomba kumegewa ardhi katika maeneo ya hifadhi ya mapori yaliyopo jimboni kwake.

Awali, akitoa ufafanuzi kuhusu ombi la Mhe.Kamwelwe la kuongezewa hekta elfu 15 katika Pori la Akiba Inyonga, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Angellah Kairuki, amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea maombi hayo na inaendelea kufanya tathimini kuangalia uhitaji halisi na kuyawasilisha kwa mamlaka kwa hatua zaidi.