Back to top

Ajali ya basi la Zuberi Express Shinyanga.

15 June 2022
Share

Taarifa ya awali: Watu watatu akiwemo dereva aliyetambulika kwa jina la Hamza Kitima wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya basi lenye namba T 435 DJS mali ya kampuni ya Zuberi Express kumepata ajali baada ya kugonga ukingo wa daraja katika eneo la Mwigumbi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kiando amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo cha ajali inasemekana dereva alipata tatizo la kiafya wakati akiwa safarini na hii ni kwa mujibu wa mashuhuda ambao walikuwa ni abiria hivyo uchunguzi wa kina wa ajali hiyo unaendelea.

Kamanda Kiando ametoa wito kwa madereva kufanya uchungizi wa afya zao kabla ya kuanza safari na endapo dereva atajihisi hayuko sawa kiafya asilazimshe kuendesha gari.