Back to top

AJALI YAUA MADEREVA NA KUJERUHI MMOJA LINDI

14 July 2024
Share

Ajali iliyohusisha magari mawili ya kampuni ya  Specialized Hauliers  pamoja na kampuni ya saruji ya Dangote, yamegongana na kusababisha vifo vya madereva wa magari yote mawili, na majeruhi mmoja mkoani Lindi.

Ajali hiyo imehusisha gari namba T 393 DKA aina ya  Howo mali ya kampuni ya Dangote, lililokuwa  likiendeshwa na Daudi Mdota  (40) iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea  Mtwara, kugongana na gari namba T 234DZ T aina  ya Howo mali ya kampuni ya Specialized Haulers LTD lilokuwa linaendeshwa na Jafari Omari.

Chanzo cha ajali kimetajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari namba T 393 DKA HOWO  kutokuwa makini kwa watumiaji wengine wa barabara kwa kuhama upande wake wa kushoto na kuhamia kulia.

Miili ya marehemu imepelekwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Lindi, Sokoine kuhifadhiwa,  pamoja na majeruhi aliyejulikana kwa jina la Saidi Mussa,  ambae  ameungua maeneo mbalimbali ya mwili wake nae akipelekwa hospitalini hapo  kwa matibabu zaidi.