Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kutoka Kikosi 514 KJ, kilichopo wilayani Makambako mkoani Njombe, wametakiwa kufuata sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Usalama Barabarani wa Mkoa huo, Mrakibu wa Polisi, Jane Warioba, alipozungumza na Maofisa na Askari wa kikosi hicho, ambapo amewataka kupata mafunzo ya udereva na kuwa na leseni za udereva kwa mujibu wa sheria.
.
Aidha, amewafundisha itifaki na udereva wa kujihami wakati wakiwa na viongozi na jinsi ya kuchukua tahadhari wanapotumia vyombo vya moto kwa kuwajali watumiaji wengine wa barabara.