Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) yaanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa njia ya mtandao.
Dirisha la kuwasilisha rufaa hizo litakuwa wazi kwa siku tano, kuanzia leo Jumatano 21 Novemba 2018 hadi Jumapili, Novemba 25, 2018 na linapatikana kupitia tovuti ya bodi hiyo ambayo ni http.olas.heslb.go.tz..
Imeelezwa kuwa HESLB imefungua dirisha hili ili kutoa fursa kwa wanafunzi wahitaji ambao hadi sasa hawajapata mkopo au hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa, kuwasilisha maelezo na nyaraka kuthibitisha uhitaji wao. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kuwasilisha na nyaraka zinazohitajika yanapatikana kwenye mtandao (http.olas.heslb.go.tz) na Wanafunzi watakaokua wametimiza masharti na sifa watapangiwa mikopo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Novemba, 2018.