Zaidi ya wanafunzi 59,000 wameandikishwa darasa la awali katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro kwa mwaka 2017 /18 kutoka wanafunzi 49,000 kwa mwaka 2015/16 hali inayopelekea wanafunzi hao kupokezana kwenye vyumba vya madarasa kwa ajili ya kusomea huku halmashauri hiyo ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa 1300.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu ambayo kwa halmashauri ya manispaa ya Morogoro yameadhimishwa katika viwanja vya K/Ndege afisa elimu msingi Abdul Buhet amesema kuwa ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi kwa darasa la awali limepelekea upungufu wa vyumba vya madarasa.
Kwa upande wao walimu ambao walishiriki maadhimisho hayo nao wakaelezea maadhimisho hayo ya wiki ya elimu huku wakiomba wazazi kuwasimamia wanafunzi pindi wanaporudi nyumbani wakati wa likizo.
Maadhimisho ya wiki ya elimu katika halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yameambatana na utoaji wa zawadi kwa walimu wa kuu wa shule zilizofanya vizuri katika taaluma.