Back to top

INTANETI YAENDELEA KUZIMWA BANGLADESH

23 July 2024
Share

Huduma ya Mawasiliano ya Intaneti, imeendelea kuzimwa nchini Bangladesh kwa siku ya tano mfululizo huku serikali ikitangaza leo kuwa siku ya mapumziko.

Mamlaka za nchi hiyo zimeendelea kudhibiti hali ya usalama licha ya kurejea utulivu kiasi baada ya mahakama kutoa amri ya kuondolewa mfumo wenye utata wa kugawa nafasi za ajira za serikali,na ambao ulichochea maandamano makubwa ya vurugu nchini Bangladesh.

Kwa siku kadhaa nchi hiyo iko chini ya amri inayokataza watu kutembea nje na wanajeshi wamekuwa wakionekana wakipiga doria katika mji mkuu na maeneo mengine.

Machafuko makubwa yameshuhudiwa kati ya polisi na waandamanaji wengi wanafunzi wanaotaka uondolewe mfumo unaotenga asilimia 30 ya ajira za serikali, kwa kwaajili ya familia za wanajeshi wakongwe waliopigana vita vya kudai Uhuru wa Bangladesh mwaka 1971.