Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaonya wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya mazoezi ya kijeshi kuacha tabia ya kuvamia maeneo hayo kwakuwa wanakwamisha shughuli za jeshi na kuhatarisha usalama wao kwakuwa maeneo hayo ni maaalum kwaajili ya mazoezi ya silaha za kijeshi
Mkuu wa mafunzo mtandaji kivita wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jeneral Alfredy Kapinga ametoa kauli hiyo wilayani Monduli mkoa wa Arusha katika hitimisho la zoezi la medani kwa onesho la shambulio la kunuia mchana lililohusisha silaha nzito za kivita vikiwemo vifaru, rocket ranger, mizinga pamoja na zingine kwa zaidi ya askari wanafunzi mianne kundi maalum la nne mwaka 2020.
Mkuu wa shule ya awali ya mafunzo ya kijeshi ya RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala amesema vijana hao wa kundi maalum waliofanya vizuri kwenye mchepuo wa sayansi watasaidia kulibadilisha jeshi la Tanzania.