#LEOKATIKAKUMBUKUMBU: Usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, Meli ya MV Bukoba ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.
Katika ajali hiyo watu 114 waliokolewa wakiwa hai wakati miili ya watu 391 iliopolewa kutoka majini na kuzikwa katika makaburi ya pamoja yaliyopo Igoma Jijini Mwanza barabara ya ya kwenda Musoma. Miili mingine ilichukuliwa na ndugu pamoja na jamaa zao kwa ajili ya taratibu za mazishi. Jumla ya miili 282 haikupatikana.
Mungu aendelee kuwapumzisha wale wote waliopoteza maisha siku ya 21 Mei 1996 katika ajali ya Meli ya Mv Bukoba.