Back to top

MAKANDARASI ZINGATIENI KANUNI, TARATIBU NA SHERIA

25 September 2024
Share

Makandarasi nchini wametakiwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zinazoongoza shughuli za ujenzi, ikiwa ni pamoja na kulipa ada za mwaka za usajili, kusajili miradi ya ujenzi ambalo ni takwa la kisheria na kuzingatia usalama wa maeneo ya kazi.

Hayo yamebainishwa na Msajili Msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) Mhandisi. David Jere, wakati wa kufungua mafunzo ya Mipango na Udhibiti wa Miradi ya Ujenzi yanayofanyika kwa muda wa siku tatu, amesema lengo la mafunzo hayo ni kukuza ujuzi kwa makandarasi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi kuanzia mipango mizuri, mbinu za utekelezaji na mambo yote yanayowezesha mradi kutekelezwa kwa ufanisi.
 
Kwa upande wake Mkandarasi Joseph Mataluma, amesema ana matumaini kupitia mafunzo hayo atajifunza namna mkandarasi, anavyotakiwa kuusimamia mradi kuanzia hatua za mwanzo hadi kukamilika ukiwa kwenye ubora na viwango vinavyohitajika.

Mafunzo haya yamewakutanisha washiriki zaidi ya 140 kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini.