Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa na bendera ya Kenya kupepea nusu mlingoti kwenye majengo na ofisi zote za umma, Jeshi na Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo kote duniania kufuatia kifo cha Rais wa pili wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi aliyefariki Nairobi Hospital alikokuwa akipatiwa matibabu leo asubuhi Februari 04, 2020.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ikulu ya Kenya inaeleza kwamba Muda wa maombolezo hayo utakoma baada ya mazishi ya Mzee Moi, hata hivyo Mpaka sasa ratiba ya mazishi bado haijawekwa hadharani.
Marehemu Daniel Arap Moi alizaliwa 1924 na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani (1964), Makamu wa Rais (1967 - 1978), Agosti 22, 1978 akawa Rais wa Kenya hadi Disemba 30, 2002, ambapo amefariki akiwa na umri wa miaka 95.