
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki kwa watoa huduma na ndugu wa wagonjwa katika mazingira ya Hospitali, (Upanga na Mloganzila) ikiwemo wodini na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma (MNH), Bw.Aminiel Aligaesha katazo hilo linatolewa kufuatia uwepo wa mifuko ya Plastiki, kwenye mazingira ya hospitali iliyopigwa marufuku na Serikali .
Aligaesha amesema katazo hilo linaanza mara moja na ni kwa kampasi zote mbili za Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambazo ni Upanga na Mloganzila.