Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Mwanza zabomoa uzio wa makabauri ya pamoja ya waliofariki Dunia katika ajali ya MV Bukoba yaliyopo katika eneo la Igoma na kuharibu baadhi ya makaburi.
Ajali ya meli ya MV Bukoba ilitokea Mei 21, 1996, eneo ambalo limekua likitumika kama kumbukumbu ya ajali hiyo iliyopoteza watu zaidi ya 800.
Kubomoka kwa uziohuo kutokana na mvua zinazonyesha kumechangia kuharibu miundombinu ya makuburi hayo hali iliyo sababisha wananchi kupaza sauti zao ili eneo hilo lenye kumbukumbu muhimu kwa taifa ifanyiwe marekebisho.
Akizungumza na ITV Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba amesema tayari wameshaanza kufanya tathmini ili kuanza ujenzi.
Miili ya watu 391 ambayo haikutambuliwa ama kuchukuliwa na ndugu zao ilizikwa katika makaburi hayo ya pamoja eneo la Igoma.