Back to top

NECTA yatangaza kuanza kwa mitihani ya darasa la saba Septemba Tano.

04 September 2018
Share

Baraza la mitihani limetangaza kuanza kwa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kuanzia kesho jumatano  utakaohusisha wanafunzi wapatao 960,202 huku kukiwa na mabadiliko katika mfumo ,wakipunguza baadhi ya maswali kutoka hamsini mpaka arobaini na tano.

Akizungumza kuhusiana na mfumo huo ambapo kwa sasa kutakuwa na  maswali matano ya kujieleza tofauti na awali ambapo maswali yote yalikuwa ya kuchagua katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt.Charles Msonde amesema hiyo ni katika kuboresha zaidi.

Aidha Dkt. Msonde  amezitaka kamati za mitihani za mikoa, halmashauri, na manispaa kuhakikisha taratibu zote zinazingatiwa za usalama na amani pamoja na kuhakikisha udanganyifu unadhibitiwa.

ITV imepita katika shule mbalimbali na kukuta wanafunzi wakiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea mtihani huo.