Back to top

Polisi Arusha yatoa taarifa za awali juu ya ajali iliyoua watu 6

02 September 2018
Share

Jeshi  la  polisi  mkoani   Arusha  limetoa  maelezo  ya  awali  ya chanzo  cha  ajali  mbaya  iliyotokea eneo  la  mti  mmoja  wilayani  Monduli   na  kusababisha  vifo  vya watu   sita  wakiwemo   raia  watatu  wa  kigeni  na  wengine  watatu  kujeruhiwa.
 
Akizungumza  ajali  hiyo  kamanda  wa  polisi   wa  mkoa   wa  Arusha  Ramadhani  Nga’nzi  pamoja  na kutoa taarifa  hiyo  pia  amesema  taratibu  za  kuwatambua  marehemu   na  nchi   wanakotoka zinaendelea.

Majeruhi  walionusurika kweye  ajali  hiyo   ambao   wamelazwa kwenye  hospitali  ya  mkoa  wa  Arusha ya  Mount  Meru  na  wengine  hospitali  ya   Lutheran  ya Arusha  ambao  walikuwa kwenye lori wamesema  gari  lao  lilipata hitilafu  kwenye  mfumo  wa  breki.

Kaimu  mganga  mkuu  wa  hospitali  ya mkoa  wa Arusha ya  Mount  Meru  Dkt. Othumani  Chande  na  Dkt. Peter  Mabula  wa  hospitali  ya Arusha  Luthrani   wamethibitisha  kupokea  miili  mitano  ya marehemu  waliofariki katika  eneo  la  ajali  na  kwamba  mmoja alifariki  wakati  wanapatiwa matibabu.

Mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha  Bw.  Mrisho  Gambo  wametembelea  majeruhi  na kwamba  taratibu juu ya raia  wa  kigeni waliofariki  zinaendelea .