Back to top

"Rais Magufuli alikuwa kiongozi bora wa Tanzania"Rais Xi Jinping.

24 March 2021
Share

Rais wa China Xi Jinping ametoa pole kwa Serikali ya Tanzania, Familia ndugu Jamaa na Marafiki kufuatia kifo cha Hayati Rais Dk.John Pombe Magufuli, huku akisema Rais Magufuli alikuwa kiongozi bora wa Tanzania.

Amesema Hayati Rais Dk.Magufuli ametoa mchago mzuri kukuza ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Tanzania na kati ya China na Afrika wakati wa uhai wake.

Ameeleza kuwa Kifo cha Hayati Rais Magufuli nipigo kwa Tanzania lakini pia kwa China kwani wamepoteza rafiki mzuri.

Ameongeza kuwa China ipo tayari kufanya kazi na Tanzania ili kuimarisha ushirikiano wa pande zote mbili pamoja na watu wake.