Back to top

Rais Magufuli awapa majukumu TAKUKURU.

14 October 2019
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi kwa miradi 107 yenye thamani ya shilingi Bilioni 90.28 iliyobainika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu (2019) kuwa na dosari mbalimbali zikiwemo kutekelezwa chini ya ubora, kutokamilika, matumizi mabaya ya fedha za umma na udanganyifu.

Mhe.Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 14 Oktoba, 2019 katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika Kitaifa katika uwanja wa Ilulu Mjini Lindi.


Mhe. Rais Magufuli amekabidhi kitabu cha taarifa ya miradi hiyo kilichowasilishwa kwake na Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu Bw.Mzee Mkongea Ali kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen.John Mbungo na kumuagiza wote wakaobainika kuhusika katika dosari za miradi hiyo kufikishwa Mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake.

Katika taarifa hiyo Bw.Mzee Mkongea Ali amesema udanganyifu mkubwa umebainika katika miradi ya maji na amesisitiza kuwa endapo fedha nyingi zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kutatua tatizo la maji zitasimamiwa vizuri, tatizo hilo litapata ufumbuzi.
[20:21, 14/10/2019] Anna Malya: okk