Back to top

Rais Samia mgeni rasmi katika mapokezi ya ndege mpya Kesho.

29 July 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mapokezi ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya De Havilland Dash 8 q400 inayotarajiwa kuwasili kesho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Akizungumza jijini Dar es salaam Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk Leornard Chamuriho amesema ndege hiyo ambayo imetengenezwa nchini Canada itawasili majira ya mchana.

Ndege hiyo inakuwa ndege ya tano kwa kundi la ndege za masafa mafupi na kufanya  idadi ya ndege kufikia tisa kati ya 11 zilizonunuliwa na serikali ambapo mbili zilizobaki zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwaka huu.