Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema kuanzia sasa mfugaji yeyote atakaethubutu kulisha mifugo yake kwenye shamba la mkulima, serikali itachukua hatua kwa kukamata na kutaifisha mifugo hiyo, vivyo hivyo adhabu kama hiyo itakuwa kwa wakulima watakaokwenda kinyume kwa kudhuru mifugo na kusababisha migogoro.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ambapo ameeleza kusikitishwa na uwakilishi hafifu wa wajumbe hasa wabunge , wakati maamuzi yanayofikiwa yanawahusu wananchi wanaowaongoza.