Back to top

SUALA LA KUPANDA MITI NI LAZIMA"DK.MPANGO

27 March 2023
Share

Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango, amesema suala la kupanda miti ni lazima na kuzitaka Halmashauri zote nchini kusimamia kwa karibu na kuhakikisha kwamba mazingira ya maeneo yao yanakuwa ya kijani, safi na ya kuvutia na zoezi hilo liwe endelevu.

Makamu wa Rais ameeleza hayo wakati wa akizundua kampeni ya kupanda miti kitaifa kwa hisani ya Benki ya NMB, ikishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wanapaswa kutoa maelekezo kwa shule, taasisi mbalimbali na kwa wananchi ili washiriki kikamilifu katika uhifadhi na usafi wa mazingira.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Serikali inafahamu na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi pamoja na taasisi za kidini hapa nchini katika kuhakikisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira inakuwa na mafanikio. 

Pia ametoa wito kwa taasisi hizo kuongeza juhudi hasa katika kuhamasisha, kukuza uelewa na kujenga uwezo wa jamii na taasisi mbalimbali kuhusu hifadhi ya mazingira pamoja na kutafuta rasilimali fedha zitakazo changia utekelezaji wa Sera ya Mazingira.

Ametoa rai kwa Benki ya NMB kuona uwezekano wa kutumia umoja wa Mabenki (TBA) kuongeza nguvu zaidi katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa muda mfupi zaidi kwa kutambua ndio makao makuu ya nchi.