Back to top

TAKUKURU Mkoani Shinyanga yarejesha nyumba ilioporwa kwa mkopo umiza.

14 January 2021
Share

Taasisi Ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imerejesha nyumba ya marehemu Sajent Edward Mpolosi kwa familia yake baada ya kuwa imechukuliwa kwa madai ya kushindwa kurejesha mkopo umiza wa shilingi 300,000 na riba kufikia kiasi cha shilingi milioni 10,500,000 hali ambayo imesababisha adha na changamoto ya usumbufu kwa familia hiyo kwa kukosa mahali pakuishi baada ya baba yao kufariki dunia.
.
Akitoa taarifa hiyo Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kahama Frank Masilamba kwa niaba ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga amesema nyumba hiyo ilikuwa kiwanja  namba 165 Kitalu  J, Mtaa wa Nyihogo wilayani Kahama.