Kuelekea Mchezo wa Simba na Yanga, Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku watu kuingia uwanjani na silaha huku likisema limejiimarisha kiusalama, na kuonya watoto wadogo kwenda uwanjani.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ACP) Muliro Jumanne Muliro.