Kiwango cha uharibifu wa misitu hapa nchini kimeongezeka na kufikia hekta lakini nne na elfu sitini na tisa kwa mwaka na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya tano duniani kwa kuwa na kiwango cha juu cha upotevu wa misitu.
Kauli hiyo imetolewa wilayani Mufindi na Frank Luvanda Katibu mtendaji wa mtandao wa asasi za mazingira Tanzania (MA-NET) .
Bwana Luvanda amesema kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha serikali cha kufuatilia mabadiliko ya tabia nchini kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo cha Morogoro kiwango cha uharibifu na upotevu misitu kinasababishwa na kilimo cha kuhamahama na shughuli zingine za kibinadamu.