Back to top

Vijana wadaiwa kutumia sumu ya panya kama mbadala wa madawa ya kulevya

27 March 2019
Share

Serikali imebaini mbinu  mpya ya vijana kutumia sumu ya panya na dawa za usingizi  kama mbadala wa madawa ya kulevya baada ya serikali kudhiti biashara ya uingizwaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.

Akizungumza na vijana wa skauti mkoani Kilimanjaro Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera ,bunge kazi ajira na watu wenye ulemavu Mh.Jenista Mhagama  amesema asilimia kubwa ya vijana kwa sasa wamebianika kutumia kemikali za sumu baada ya serikali kudhibiti biashara ya madawa ya kulevya kwa asilimia 90.

Amesema asilimia 56 ya nguvu kazi hapa nchini ni vijana na kwamba kama hatua za kudhibiti kundi hili kubwa  lisiendelee kuathiriwa na madawa ya kulevya kuelekea uchumi wa kati kuna hatari ya kukosa vijana watakaokuwa na uwezo wa kufanya kazi .

Kwa upande wake Kamishna wa skauti mkoa wa Kilimanjaro Bw.Brighton Matola  amesema vijana wengi kwa sasa wanatumia madawa mbadala kuvuta na kujidunga hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kuwadhibiti  licha ya kuendelea kutoa elimu kwa vijana kuhusu madhara ya madawa ya kulevya.

Mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi Dr.Japhet Boniface amesema madawa ya kulevya yamekuwa na athari kubwa kwa vijana  baada ya kuvuta kemikali hizo husababisha ubongo kupata madhara pamoja na miili yao kudhoofu na hivyo kuwapelekea kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.