Wananchi wa kijiji cha Ligoma wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuwajengea daraja baada ya daraja wanalolitumia la Ligoma kuharibika na kuhatarisha maisha yao hasa ya wanafunzi pindi maji yanapofurika kwenye mto Ligoma.
Wakizungumza na ITV katika kijiji cha Ligoma wananchi hao wanasema licha ya adha wanayoipata lakini pia wanashindwa kusafirisha mazao yao kutokana magari na piki piki kushindwa kupita kwenye daraja hilo na hivyo wanalazimika kupita bara bara ya kuzunguka kupitia kijiji cha Msinji ambako wanatumia gharama kubwa.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ligoma Bw. Abdalah Jalasi anasema wananchi wa kijiji cha Ligoma wamelazimika kuliunganisha daraja hilo na miti ili waweze kupita kwa miguu ambapo mvua zinapozidi mawasilino kati ya kijiji cha Ligoma na vijiji vingine yanakatika