Back to top

WANAUME MBULU WATAKIWA KUFUNGUKA WAKIPIGWA.

23 December 2022
Share

Wanaume wilayani Mbulu mkoani Manyara, wametakiwa kufunguka na kutumia dawati la jinsia na watoto kutoa taarifa, pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kupigwa na wake zao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Maria Nzuki, wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, zilizojengwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu na Afya ya uzazi (UNFPA) kwa kushirikiana na Shirika la Utu wa Mtoto (CDF).

DCP Nzuki alisema Wanaume wengi wamekuwa wakiona aibu kuripoti matukio hayo, katika dawati jambo ambalo limekuwa likiendeleza vitendo hivyo katika jamii, hivyo ili kukomesha tabia hiyo wanapaswa kutoona aibu.