
Watu 3 wamethibitika kufariki dunia nchini Kenya, baada ya jengo la ghorofa 7 kuanguka kwenye eneo la Karasani Kaunti ya Nairobi na juhudi za kuokoa wengine zikiendelea, huku watu 7 waliookolewa wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.
Maafisa wa KDF wanaendelea na zoezi la uokoaji huku wakifukua vifusi vya jengo hilo ambalo lilikua bado linajengwa kabla ya kuanguka.
Mamlaka ya ujenzi nchini humo imesema mmiliki wa jengo hilo alikua ameonywa kuhusu uhafifu wa jengo hilo, ila alikaidi kusimamisha ujenzi.