
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameviagiza vyombo vya dola kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli zake ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.
Dk. Gwajima ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama ambapo amesema kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo ambalo limekuwa likiivuruga wizara yake na serikali kwa ujumla katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.