Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, kwa kuweka taa za barabarani baadhi ya maeneo ya Ruangwa mjini.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, amesema toka kuwekwa kwa taa katika maeneo mbalimbali ya Ruanga Mjini wananchi wamekuwa wakifanya mazoezi usiku.
“Lakini niwapongeze Ruangwa sasa inang'ara ikifika usiku,hongereni, Tabora wamejipambanua wao wanasema Toronto na sisi siku hizi ni New York”.
Mji kwa kweli unang'ara nyakati za usiku na yeye anatamani achelewe chelewe tu ili apite usiku ili aone Ruangwa inafananaje usiku, ambapo siku hizi watu wa pikipiki wanatembea bila kuwasha taa mpaka Kitandi.
Amesema siri kubwa ambayo sasa anaiyona ni mahusiano mazuri yaliyomo kwa watumishi wa Serikali kwenye ofisi zote za serikali, saivi mnazungumza lugha moja ofisi ya mkuu wa wilaya na ya mkurugenzi lakini pia ameona mahusiano yao hadi chamani hakuna migogoro.
Zamani ilikuwa watu wanatega yaani wanamtega mtu ili akikosea tu wamshughulikie lakini ile siku hizi haipo.